Waitaliano
wameitumia katuni ya wachezaji wanne wa England wakiwa kwa mganga wa kienyeji.
Mganga
huyo anaonekana ni Andrea Pirlo, mkongwe anayekipoga Juventus na timu yao ya
taifa ya Azzuri.
Pirlo
anaonekana akiwa tiba Raheem Sterling, Theo Walcott, Jordan Henderson na Danny
Welbeck.
Lengo
la Waitaliano ni kuonyesha Pirlo akiwapa tiba vijana hao waisaidie England.
Lakini Waingereza wameona ni kama kubezwa.
Nao
wakatupia picha mtandaoni Sterling akiwa amemlaba chenga Pirlo hadi akaanguka.
Sasa
wanahoji: “Mganga wa aina gani anayetibiwa na mgojwa wake?”
Basi
raha tu, kweli mpira haushi vituko na sasa mashabiki hao wanaendelea kulumbana
kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter na Instagram.









0 COMMENTS:
Post a Comment