Mshambuliaji
mpya wa Manchester City, Raheem Sterling amesema kuondoka kwake Liverpool
hakukuwa na nia ya kuwaumiza mashabiki wa klabu hiyo.
Sterrling
amejiunga na Man City akitokea Liverpool kwa dau kubwa zaidi la pauni milioni
49 ambalo ni rekodi ya juu ya usajili kwa Waingereza.
Mashabiki
wa Liverpool wamekuwa wakimzomea Sterling kila wanapomuona, jambo lililoonyesha
kumuumiza.
“Najuta, najisikia vibaya maana halikuwa
lengo langu kuwakasirisha,” alisema Sterling.
Ilifikia
Sterling alikataa kuongeza mkataba Liverpool baada ya kuwa wamempa mkataba mpya
wenye mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki.









0 COMMENTS:
Post a Comment