July 30, 2015



BAADA ya mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva kushindwa kung’ara katika michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi hapa nchini, amedai kuchanganyikiwa na kujiona ni mwenye wakati mgumu klabuni hapo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Msuva alisema anajisikia vibaya sana kwa sasa kwani hakutarajia kabisa kukumbana na hali hiyo ambayo sasa inamuumiza kichwa na kumweka kwenye wakati mgumu.

 “Hata hivyo sina jinsi, imeshatokea, ninachotakiwa kwa sasa ni kujipanga upya ili kuhakikisha narudisha kiwango changu kama ilivyokuwa msimu uliopita.

“Nitaanza moja kabisa japokuwa akili yangu kwa sasa nahisi kama imechanganyikiwa, nilitarajia kupata nafasi na kuonyesha kiwango kizuri lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo,” alisema Msuva.


Msuva ambaye aliibuka mfungaji bora wa michuano ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita baada ya kuzifumania nyavu mara 17, alishindwa kung’ara kabisa katika michuano hiyo ya Kombe la Kagame na kujikuta akiondolewa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo ambacho juzi Jumatano kulitupwa nje ya mashindano hayo na Azam FC.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic