BEKI kisiki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amefunguka kwa kusema kuwa wametolewa kihalali katika michuano ya Kombe la Kagame na bahati haikuwa kwao.
Yanga ilijikuta ikiondolewa katika Kombe la Kagame, juzi, kwenye hatua ya robo fainali dhidi ya Azam FC kwa mikwaju ya penalti 5-3.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Cannavaro alisema kuwa hawawezi kumlaumu mtu kwani walichokosa ni bahati tu ndani ya dakika tisini.
“Siwezi kusema kuwa Azam ndiyo timu bora zaidi yetu, kwani tuliwazidi uwezo kwa jinsi tulivyocheza, lakini Mungu hakutujaalia kuweza kusonga mbele na hatuwezi kumlaumu mtu katika hili kwani tumetolewa kwa bahati mbaya.
“Kwa sasa tunajiandaa kwa ajili ya ligi baada ya mapumziko mafupi kwa kuhakikisha tunajifua kwa nguvu zote ili tuweze kufanya vizuri,” alisema Cannavaro.
0 COMMENTS:
Post a Comment