Kiungo Kipre Bolou anasafirishwa kwenda
nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kupata matibabu.
Bolou raia wa Ivory Coast amekuwa majeruhi
kwa muda mrefu sasa, hali iliyofanya uongozi wa Azam FC kumpa matibabu zaidi.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga
amesema kiungo huyo atakuwa nchini humo kwa zaidi ya wiki mbili.
“Kweli anakwenda kwa matibabu, inawezaa
kuwa wiki mbili au zaidi lakini kikubwa ni suala la matibabu yatakavyokuwa,”
alisema.
Bolou ni ndugu wa Kipre Tchetche,
mshambuliaji wa Azam FC pia ambaye msimu huu anaonekana kurejea.
0 COMMENTS:
Post a Comment