August 5, 2015

KOMBE LA KAGAME
Na Saleh Ally
Michuano ya Kombe la Kagame imefikia tamati, tayari bingwa amepatikana ambaye ni Azam FC, hongera kwao.


Kati ya changamoto ambayo ialianza kuzungumziwa tokea awali ni fedha za zawadi kwamba dola 30,000 kwa bingwa, 20,000 kwa mshindi wa pili ana 10,000 kwa mshindi wa tatu huwa haziongezeki.

Hilo lilionekana kuwazidi nguvu Cecafa na swali likawa hivi, siku akijitoa Rais Paul Kagame itakuwaje?
KOMBE LA BINGWA WA NDONDO CUP ARUSHA

Lakini wakati hayo yamepita, changamoto iliyozua gumzo tena ni kombe ambalo alikabidhiwa bingwa Azam FC.

Kombe limekuwa ni sehemu ya kuonyesha hadhi ya mashindano husika.

Kombe la ubingwa wa Kagame ambao ni ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa klabu bingwa kwa nchi linaonekana kuwa na hadhi ya chini hata kuliko yale yaliyotolewa katika mechi za michuano ya mchangani maarufu kama ndondo?

Kombe hilo ni dogo, la kawaida, halina hadhi na huenda limekuwa likitoa picha namna ambavyo Cecafa chini ya Katibu wake, Nicholas Musonye imekuwa haina maandalizi ya kutosha.

Kuna kila sababu ya kutafuta kombe ambalo litakuwa linatambulika na la aina moja kuliko kila baada ya miaka miwili linabadilishwa.
KOMBE LA UBINGWA WA MCHANGANI WA MWIDAU

Angalia Kombe la Dunia, Afcon na michuano mingine mfano Ligi Kuu England, La Liga, Seriea A, Bundesliga na mingineyo wamekuwa wakitumia kombe la aina moja ambalo linakuwa utambulisho na heshima ya michuano.


Cecafa wana kila sababu ya kufanya kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko ili kuendelea kulinda hadhi ya michuano hiyo kuliko kuwakabidhi mabingwa makombe yenye hadhi chini ya mchangani wakati mchangani wanapewa makombe yenye hadhi ya juu ya Kagame Cup.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic