Bondia
asiyepigika, Floyd Mayweather amemtosa Mwingereza, Amir Khan na sasa atapigana
na bingwa mwingine.
Hilo
litakuwa ni pambano la 49 la Mayweather ambaye hajapigwa hata mara moja na
linatarajia kufanyika Septemba 12 jijini Las Vegas, Marekani.
Mmarekani
huyo anatarajia kuzichapa na Andre Berto ambaye pia ni bingwa wa uzito huo.
Pambano
lake la mwisho lilikuwa ni dhidi ya Manny Paqcuiao na ushindi wake ulizua
mjadala mkubwa mara tu baada ya pambano kwenye ukumbi wa MGM Grand Garden Arena.
Mayweather
anakaribia mapambano 50 bila ya kushindwa na yeye amekuwa akisema kwamba
pambano lijalo ndilo la mwisho ingawa watu wake wa karibu wanasema atacheza
hadi mapambano 50.
0 COMMENTS:
Post a Comment