Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe
Magufuli amesema hatawaangusha wanamichezo pamoja na wanamuziki.
Akihutubia leo kwenye Viwanja vya Jangwani
wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za CCM, Magufuli alisema kamwe
hatawaangusha na kuwasahau.
“Najua mnahitaji maendeleo, kwa nini
Wanamuziki wa Marekani na wanamichezo wa
sehemu mbalimbali na wa hapa Tanzania wasiwe matajiri.
“Nawaahidi sitawaacha kwa kuwatumia kwenye
kampeni na siasa tu. Badala yake nitawapigania maendeleo yenu.
“Najua kila mtu anataka mabadiliko, lakini
mabadiliko yaendane na maendeleo yenu,” alisema Magufuli na kushangiliwa kwa
nguvu.
Wasanii mbalimbali wakiwemo wa Bongo Movie
na Bongo Fleva walijitokeza wakati wa kampeni hizo na kushangiliwa na umati
mkubwa wa waliojitokeza.
0 COMMENTS:
Post a Comment