August 23, 2015


Taifa Stars inaondoka kesho alfajiri kwenda nchini Uturuki kwa kambi ya wiki moja huku kocha wake akisema baridi itawasaidia wakiwa huko.


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema ana imani kubwa itamsaidia kukiunganisha kikosi chake akiwa ugenini.

"Tutakuwa na mechi mbili za kirafiki ambazo zitasaidia kujua wapi tunatakiwa kuunganisha," alisema.

"Kuna mambo kadhaa ya kuyafanyia kazi, tutakapokuwa Uturuki tutapata nafasi namna ya kufanya."

Kuhusiana na baridi, Mkwasa alisema wana taarifa ya kuwa na baridi kiasi lakini ni nzuri kwa wachezaji wake.

"Kisayansi ni bora wachezaji kufanya mazoezi kwenye baridi badala ya sehemu yenye joto. Hivyo baridi kwa kuwa si kali sana, nina imani itatusaidia," alisisitiza Mkwasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic