Akipewa mkataba wa miaka mitatu na Yanga, beki mpya wa Yanga,
Vincent Bossou, amekumbwa na balaa la kuondolewa katika kikosi cha timu hiyo
kitachocheza katika michezo ya Ligi Kuu Bara na kupelekwa katika michezo ya
kimataifa.
Bossou ambaye ni raia wa Togo, ni miongoni mwa wachezaji wa
kimataifa waliosajiliwa hivi karibuni katika timu hiyo akiwa sambamba na
Thabani Kamusoko ‘Ras’ aliyesajiliwa akitokea timu ya FC Platinum ya Zimbabwe.
Yanga inatarajiwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika
msimu ujao, ikiiwakilisha Tanzania huku Azam ikishiriki Kombe la Shirikisho
Afrika.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro,
alisema kuwa lengo kubwa la kusajiliwa kwa beki huyo ni kuja kuisaidia timu
hiyo katika michezo ya kimataifa ambapo timu hiyo imekuwa ikifanya vibaya.
“Tumeamua kumsajili Bossou baada ya viongozi na benchi la ufundi
kuridhishwa na uwezo wake ambao ameuonyesha kwa siku chache ambazo alikuwa
katika kikosi chetu katika kambi yetu ya Mbeya.
“Kocha wetu, Mdachi Hans van Pluijm, amepanga kumtumia mchezaji
huyu katika michezo ya kimataifa kutokana na uzoefu wake katika michezo hii,
hasa kutokana na rekodi yake,” alisema Muro.
0 COMMENTS:
Post a Comment