Mshambuliaji Papa Niang amepewa Jumatatu kama
nafasi ya kuwadhihirishia Simba kwamba ana uwezo na atakuwa msaada, hivyo chaguo lake, ashindwe arudi Senegal, afanye vitu apande meli ya Simba.
Niang raia wa Senegal ambaye amewasili nchini
jana na kujiunga na Simba, anasubiri siku hiyo ambayo Simba itacheza na MWadui
FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kumshawishi kocha Dylan Kerr na
benchi zima la ufundi kwamba anaweza.
Lakini Niang ataitumia nafasi hiyo pia
kuwashawishi viongozi wa Simba kwamba wanastahili kumwaga mamilioni ili kupata
saini yake.
Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’
amesema kila kitu kuhusiana na mechi hiyo kimekamilika.
“Ni kweli mwalimu atamtumia Papa Niang ikiwa ni
sehemu ya majaribio yake mafupi na kupata uhakika kuwa ni mshambuliaji wa
kiwango tunachotaka.
“Pia tunaamini ni nafasi ya mashabiki wa Simba
kumuona mchezaji huyo na kikosi chao kwa ujumla na wanaweza pia wakawa na
mchango wao,” alisema Kaburu.
Kuhusiana na mechi kuchezwa Jumatatu, Mkuu wa
Kitengo cha Habari cha Simba, Haji Manara amesema inawezekana ikawa tofauti
lakini ndiyo mabadiliko ya kisoka duniani.
“Unajua England sasa wana mechi zinazochezwa
Jumatatu, hizo ni mechi za Ligi Kuu England. Hapa pia tutaenda tunabadilika
taratibu na itawezekana.
“Tunaamini kunaweza kuwa na usumbufu kidogo,
lakini tutaenda tunazoea. Ninachowashawishi mashabiki wa Simba, wapenda mpira
wote wafike uwanjani.
“Pia kutakuwa na nafasi ya kumuona mshambuliaji
Papa Niang akiichezea Simba, pia kupata uhakika kutokana ana uwezo wake,”
alisema Manara.
0 COMMENTS:
Post a Comment