August 22, 2015


Yanga emekubali kumuachia mshambuliaji wake, Hussein Javu arejee katika Klabu ya Mtibwa Sugar aliyowahi kuichezea siku za nyuma.


Hatua hiyo ya Yanga imemfanya Javu apagawe kwa furaha baada ya kuitafuta nafasi hiyo kwa muda mrefu bila ya mafanikio akitaka kuondoka baada ya kuchoshwa na benchi.

Javu alisema sasa anaamini atafanya vizuri baada ya kurejea tena Mtibwa Sugar.

“Nafasi hii niliitafuta kwa muda mrefu, mpaka nikataka kugombana na viongozi ambao hawakutaka niondoke huku wakijua nakaa benchi, ila kwa uamuzi huu nawashukuru sana.

“Unajua nilikuwa chaguo la tano kikosini, unadhani ningecheza lini? Kila nikijitahidi wapi, bora nimeondoka,” alisema Javu.


Javu alikuwa anakumbana na changamoto ya kuwania nafasi na mastraika kama Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Malimi Busungu na wengine wasio rasmi kama Simon Msuva na Deus Kaseke.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic