August 22, 2015


Mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga dhidi ya Azam FC, hadi sasa ni mapumziko na hakuna timu ambayo imeona lango la mwenzake.



Mechi hiyo imekuwa na ushindani mkubwa huku kuila upande ukionekana kuwa umejiandaa vilivyo na kufanya mashambulizi yawe ya zamu.

Azam FC ndiyo ilionekana kushambulia zaidi katika dakika 15 za mwanzo na kuwapa wakati mgumu Yanga huku Kipre Tchetche akionekana kuwa mwiba.

Nahodha wa Azam FC, John Bocco alipoteza nafasi mbili ambazo kama angetulia, angalau angeifungia Azam FC bao moja.

kuanzia dakika ya 20, Yanga walizidi kubadilika na kuanza kuwapa Azam FC wakati mgumu huku Geofrey Mwashiuya, Simon Msuva na Donald Ngoma wakiwapa mabeki wakati mgumu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic