Na Saleh Ally
Unaweza ukaona ni kama miujiza lakini
ndiyo hali halisi kwamba lundo la wakazi wa jijini la Dar es Salaam, hasa
wapenda michezo wamelazimika kupanda vitandani na kulala.
Wapenda michezo hao wa Dar es Salaam na
sehemu nyingine za hapa nchini (Tanzania), wamelazimika kulala na huenda
watapata fursa ya kuota wakiangalia mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya ambazo
zinaendelea sasa.
Wengine wao, watalazimika kuota kwa kuwa
maeneo mengi ya Dar es Salaam na sehemu nyingine nchi hakuna umeme kutokana na
mambo ya kubahatisha ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Tanesco ilahidi kuwepo kwa matengenezo
ya siku saba la limekuwa likikata umeme mchana kutw na kurudisha usiku.
Lakini ghafla, shirika hilo ambalo
linaongoza kwa kulaumiwa na wananchi kutokana na huduma zake mbovu huenda
kuliko lingine lolote nchini sasa linakata umeme hadi usiku.
Mfano mzuri ni maeneo ya Sinza ambazo
pamoja na umeme kutokuwepo mchana wote, ulirejeshwa saa 12 jioni kabla ya
kukatwa tena saa 1 usiku, hadi sasa.
Mechi hizo za Ligi ya Mabingwa Ulaya
kama ile ya Chelsea vs Maccabi Haifa, AS Roma vs Barcelona, Dinamo Zagreb vs Arsenal
zinaendelea na wachache hasa watakaokwenda kwenye baa au kumbi za starehe
zinazomiliki jenerata ndiyo watakaobahatika kuona.
Achana na kuzorotesha maendeleo kutokana na kukata umeme hovyo, Tanesco
imekuwa ni tatizo na karaha kubwa kwa wapenda michezo kwa kuwa hata mechi za
Ligi Kuu Bara zilizochezwa leo, wengi hawakuziona.
Pamoja na kuwa na bahati kwa runinga ya
Azam TV kuonyesha Live tena kwa picha zilizo na ubora wa juu, lakini Watanzania
wengi wamelazimika kusikiliza kwenye redio.
Yote hiyo imetokana na matatizo hayo ya
Tanesco ambayo haijawahi kumaliza marekebisho, haijawahi kuwa na ahadi sahihi,
haijawahi kusema kauli zinazolingana na matangazo yake, huku likiongoza kwa kuomba radhi
kila mara kutokana na kuboronga huenda kuliko shirika jingine lolote nchini.
Tanesco ni kero
Tanesco ni adui wa maendeleo
Tanesco ni adui wa michezo
0 COMMENTS:
Post a Comment