TEGETE |
Kocha Mkuu wa Toto African, John Tegete amempigia
mwenzake wa Mwadui FC na kumwambia awe makini atakapotua Tanga.
Mwadui FC imeanza safari kwenda Tanga kucheza na
Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Jumamosi.
Tegete amemuambia Julio pale Mkwakwani kuna tabia ya
vyumba kupuliziwa dawa za kuchosha misuli, hivyo Mwadui FC wawe makini.
“Kweli alinipigia, kanieleza kuhusiana na hilo. Lakini
nimeshangaa sana kwa kuwa nimekuwa Tanga hapo kwa vipindi tofauti.
JULIO |
“Unakumbuka niliwahi kuinoa Coastal Union, halafu
nikarudi katika kipindi cha kuikomboa isiteremke daraja. Sikuwahi kuona hayo
mambo.
“Lakini tunasafiri na watu wetu akiwemo daktari,
watalifanyia hilo kazi kama kweli lipo,” alisema Julio.
Toto walilalamika kushitukia vyumba vyao kupuliziwa
dawa. Ingawa uongozi wa Uwanja wa Mkwakwani, ulilikanusha hilo vikali.
0 COMMENTS:
Post a Comment