September 23, 2015




Dusan Mormcilovic ameondoka nchini saa 10 alfajiri kurejea kwao Serbia akiachana na Simba.
Siku moja kabla ya kuondoka, Dusan amewatibua Simba baada ya kusema watafungwa na Yanga kwa kuwa hawana stamina.
Lakini yeye ndiye kocha wa viungo, alfajiri ya keo ameondoka kurejea kwao huku akisisitiza kwamba Simba itafungwa.
Katika mahojiano yake, amesisitiza akionyesha ni mwenye hasira, kwamba yeye si kocha wa Simba.
Hata hivyo, uongozi wa Simba haujalizungumzia suala lake ingawa imeelezwa kwamba Simba imeamua kuachana naye ili kupunguza matumizi.

Uamuzi huo umetokana na suala la kifedha ndani ya Simba kutokuwa zuri, hivyo kusubiri mambo yawe poa na kwa kuwa alishafanya kazi yake kwa wiki 10, uongozi wa Simba unaamini Kocha Mkuu, Dylan Kerr na Selemani Matola wanaweza kuiendeleza kazi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic