Viingilio vya mchezo wa watani wa jadi katika Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania utakaochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam vimetangazwa leo ambapo kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu
saba (7,000).
Katika mchezo huo kiingilio cha juu kitakua ni
shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa viti vya VIP A, Elfu Ishirini (20,000)
kwa viti vya VIP B & C, huku kiingilio cha shilingi Elfu Saba (7,000)
kikiwa ni kwa viti vyenye rangi ya Blu, Kijani na Orange.
Tiketi za mchezo ho zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa saa
2 kamili asubuhi katika vituo vifuatavyo: Karume – Ofisi za TFF, Buguruni –
Oilcom, Dar Live – Mbagala, Uwanja wa Taifa, Luther House – Posta, Ferry –
Kivukoni, Mnazi Mmoja, Ubungo – Oilcom na Makumbusho – Standi ya mabasi ya
daladala.
TFF inawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa
miguu nchin kununua tiketi katika magari yaliyopo kwenye vituo vya kuuzia
tiketi ili kuondokana na kuuziwa tiketi zisizo sahihi.
Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi wa kimataifa mwenye
beji ya FIFA, Israel Nkongo (Dsm) akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga),
Ferdinand Chacha (Mwanza) mwamuzi wa akiba Soud Lila (Dsm) wakati kamisaa wa
mchezo huo atakua Charles Mchau kutoka Kilimanjaro.
Michezo mingine ya Ligi Kuu ya Vodacom siku hiyo ya
Jumamosi itakua ni kati ya Coastal Union dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga, Maafande wa jeshi la Magereza (Tanzania Prisons)
watawakaribisha maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Sokoine jijini
Mbeya.
Maafande wa JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Stand United
katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, huku wakata miwa wa Turiani
Mtibwa Sugar watawakaribisha Majimjaji ya Songea katika uwanja wa Manungu
wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Toto Africans katika uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa michezo
miwili ambapo waoka mikate wa Azam FC watawakaribisha Mbeya City katika uwanja
wa Chamazi Complex, huku African Sports wakiwa wenyeji wa Ndanda FC kwenye
uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment