Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amekalia kuti kavu
kwa kuwa sasa taarifa zinasema uongozi wa klabu hiyo umewasiliana na kocha
mkongwe, Carlo Ancelotti.
Uongozi huo umewasiliana na Ancelotti ikiwa ni sehemu
ya kurekebisha mambo na kama Rodgers ataharibu tu, safari inamkuta.
Mambo yamekuwa hayaendi vizuri tokea kuanza kwa msimu
huu na kama atapoteza mechi nyingine, bila shaka atalazimika kuongoza njia kwa
kutupiwa virago ili kocha huyo wa zamani wa AC Milan, Real Madrid na Chelsea
achukue nafasi.
0 COMMENTS:
Post a Comment