Mshambuliaji wa Stand United, Elius
Maguri amezidi kupaa kileleni katika ufungaji bora baada ya kupachika mabao
mawili wakati wakiitandika Majimaji kwa mabao 3-0.
Stand imeshinda kwa mabao 3-0 katika
mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja Kambarage mjini Shinyanga.
Maguli sasa amefunga mabao hayo mawili
na kufikisha mabao nane.
Wachezaji wanaomfuatia wana mabao matano
ambao ni Hamisi Kiiza (Simba), Donald Ngoma, Amissi Tambwe (Yanga).
0 COMMENTS:
Post a Comment