Simba imepoteza mechi yake ya pili ya
Ligi Kuu Bara ndani ya mechi saba tu.
Simba ilipoteza mechi yake ya kwanza ikicheza mechi yake ya nne ya ligi ilipokutana na mabingwa watetezi Yanga iliyowachapa bao 2-0.
Ikiwa ugenini, Simba imekubali kipigo
cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wake Prisons ya Mbeya ambayo imetoka kupoteza
mechi yake kwa kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Stand Unitd.
Timu hizo zilimaliza kipindi cha kwanza
kwa sare ya bila bao kwenye Uwanja wa Sokoine, lakini Prisons wakafanikiwa
kupata bao katika kipindi cha pili kilichotawaliwa na ubabe na tafrani.
KIKOSI SIMBA:
Agban, Hassan Kessy, Mohammed Hussein’Tshabalala’,
Isihaka Hassan, Juuko Murishid, Justice Majabvi, Simon Sserunkuma, Awadh Juma, Pape
N'dew, Joseph Kimwaga na Peter Mwalyanzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment