Timu ya Yanga leo inashuka uwanjani
kupambana na Toto Africans ya Mwanza, katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na
ushindani mkubwa, Yanga itawakosa baadhi ya nyota wake wa kutumainiwa walioumia
wikiendi iliyopita ilipopambana na Azam FC kwenye uwanja huo.
Kutokana na hali hiyo kocha mkuu wa timu
hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, atalazimika kukipanga upya kikosi chake
tayari kwa kukabiliana na Toto Africans ambayo inafundishwa na Mjerumani,
Martine Grelics.
Nyota wa Yanga watakaoikosa mechi hiyo
ni Mbuyu Twite ambaye alipasuka juu ya jicho na kushonwa nyuzi tano baada ya
kugongwa na mchezaji wa Azam pamoja na Salum Telela ambaye anasumbuliwa na
maumivu ya kifundo cha mguu.
Akizungumza na Championi Jumatano,
Pluijm alisema kuwa kutokana na hali hiyo, hatawatumia wachezaji hao katika
mechi hiyo ya leo na badala yake nafasi zao zitachukuliwa na wengine ambao wapo
fiti.
“Nitawakosa Twite na Telela katika mechi
hiyo kutokana na kuwa majeruhi lakini nitawatumia waliopo kuhakikisha tunaibuka
na ushindi katika mechi hiyo.”
Wachezaji wanaotarajiwa kuziba nafasi
hizo ni Deus Kaseke atakayechukua nafasi ya Twite na Haruna Niyonzima
atakayechukua nafasi ya Telela.







0 COMMENTS:
Post a Comment