October 21, 2015


Kiungo wa pembeni wa Royal Eagles ya Afrika Kusini, Uhuru Selemani, thamani yake imefikia Sh milioni 125 iwapo suala la kumuuza litafikia.


Mtandao wa transfer market umempa uhuru thamani hiyo kwa kusema anaweza kuuzwa euro 50,000.

Mtanzania huyo amechukua nafasi ya pili katika wachezaji watatu wa kulipwa walio katika kikosi hicho kinachoshiriki daraja la kwanza nchini humo.

Kiungo Mnigeria, Prince Olomu amepewa thamani ya euro 250,000 ambaye ndiye ghali zaidi ya wachezaji wote wa kikosi hicho.

Mgeni anayeshika nafasi ya tatu kwa thamani ya manunuzi katika kikosi hicho ni kipa kutoka Ivory Coast, Noel Yobou ambaye amepewa euro 25,000 ikiwa ni nusu ya thamani ya Uhuru.


Uhuru anaichezea timu hiyo ya jijini Darbun kwa mkopo akitokea Jomo Cosmos.

1 COMMENTS:

  1. Keep It Up..... Uhuru Selemani. Hapo Bongo kipaji chako kilikuwa kinafujwa tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic