Uongozi wa
klabu ya Arsenal imeingia matatani na wanamazingira wa England ambao wamepinga
kitendo cha timu yake kusafiri kwa dakika 14 leo wakati wakienda kuivaa Norwich
katika mechi ya Ligi Kuu Engaland itakatopigwa kesho.
Kundi hilo la
wanamazingira ambalo liliwahi kuingia mzozo na Arsenal mwaka 2012 baada ya
kusafiri na ndege kwa maili 100 tu, limesema huo ni uharibibu mkubwa wa
mazingira.
Hata hivyo,
Kocha Mkuu, Arsene Wenger amesema wasingeweza kusafiri kwa basi kwa kuwa
wangekutana na vizuizi vingi vya barabara kwa kuwa iko katika matengenezo.
Wenger anaamini usafiri wa basi, ungechangia uchovu kwa wachezaji wake hivyo ndege licha ya kuwa ni sehemu fupi kwa maana ya umbali, ndiyo ulikuwa usafiri sahihi.
0 COMMENTS:
Post a Comment