Azam TV jana usiku imeshinda tuzo mbili katika tamasha la tuzo za Tanzania Leadership Awards lililofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam.
Tuzo ilizobeba Azam TV ni Best Pay-TV platform in Tanzania (ndiyo runinga bora ya kulipia kwa Tanzania) na tuzo ya pili ni Best Entertainment Channel in Tanzania (Chaneli bora ya burudani).
Kwenye picha Meneja Masoko wa Azam TV, Mgope Kiwanga akipokea tuzo hizo pamoja na wadau wengine wa Azam TV.
Azam TV ambayo haina hata miaka mitatu ndiyo runinga inayokua kwa haraka zaidi kuliko nyingine zote nchini pamoja na ukanda wote wa Afrika Mashariki hivyo kufanya iwe tishio hata kwa runinga nyingine za kimataifa ambazo awali zilionekana kuwa hazina mshindani.








0 COMMENTS:
Post a Comment