December 28, 2015


Kikosi cha Mbeya City kimebadilika kabisa ukilinganisha na kile cha misimu miwili iliyopita na kimekuwa na sura nyingi mpya, kitu ambacho wadau wengi wa soka la Bongo wamekibaini.

Lakini kingine ambacho kinaweza kuwa kigeni masikioni mwako na ukakigundua leo ni kwamba, Mbeya City ya sasa inaundwa na wachezaji wengi waliowahi kuichezea Simba na hata nusu ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo inaundwa na wachezaji hao.

Golikipa wa timu hiyo ni lejendari wa Simba, Juma Kaseja, beki kisiki wa timu hiyo ni Haruna Shamte aliyetimka Simba misimu miwili iliyopita, pia kuna Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Haruna Moshi ‘Boban’ na safu ya ushambuliaji ipo chini ya Abdallah Juma.

Usimsahau nahodha wa Mbeya City, Juma Nyosso ambaye ni mchezaji halali wa timu hiyo japokuwa amefungiwa miaka miwili na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kumdhalilisha straika wa Azam FC, John Bocco, huyu naye alipata umaarufu mkubwa alipokuwa na Simba SC. 

Kwa faida yako tu, wachezaji waliobaki katika kikosi cha kwanza cha kwanza cha Mbeya City ambao walishiriki kuipandisha kutoka daraja la kwanza mpaka ligi kuu ni Hassan Mwasapili na Steven Mazanda ambaye naye kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Yanga hakuwepo kutokana na matatizo ya kifamilia.


Hata hivyo, ongezeko pia la beki Tumba Sued hivi karibuni ndani ya kikosi hicho, limechangia kuwe na wachezaji wawili waliomo kwenye ‘first eleven’ ya Mbeya City wanaotokea Coastal Union kutokana na uwepo wa Joseph Mahundi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic