December 28, 2015


Baada ya Yanga kuifunga Mbeya City mabao 3-0 juzi Jumamosi, Kocha wa Mbeya City, Meja mstaafu, Abdul Mingange, ameibuka na kusema haamini kama amefungwa labda akaangalie tena mkanda wa mechi hiyo.

Yanga na Mbeya City zilipambana juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na kuibuka na ushindi huo kwa mabao ya Mrundi, Amissi Tambwe aliyefunga mawili na Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.

 Mingange alisema hajaridhishwa na kile alichokiona mpaka atakapoenda kuangalia mkanda wa video wa mechi hiyo labda ataamini.

“Mpaka nikaangalie tena mkanda wa video wa mechi hii ndiyo nitajua kama tumefungwa kweli au tumeonewa, naamini mwamuzi hajatutendea haki hata kidogo.

“Bao la kwanza la Tambwe lilitokana na mchezaji wangu Joseph Mahundi kuchezewa faulo na Deus Kaseke, pia hata kabla ya Tambwe hajafunga kwanza aliushika mpira, lakini nashangaa mwamuzi hajalikataa bao.

"Pia mazingira ya kutolewa beki wangu, Tumba Sued kwa kadi nyekundu (ilikuwa dakika ya 57 baada ya kumpiga kichwa Donald Ngoma), sidhani kama ilitendeka haki, lakini nashangaa aliwaacha Boban (Haruna Moshi) na Yondani (Kelvin) waendelee kucheza wakati walionyesha vitendo si vya kimichezo kwa kupigana uwanjani. Kwa hiyo nahitaji kuuangalia tena mchezo huu ili niridhike na matokeo,” alisema Mingange. 



2 COMMENTS:

  1. Mimi binafsi kwa kadiri nilivyomfuatilia refa wa mechhi ya Yanga na Mbeya City hata kabla ya mechi hiyo, nilijua tu lazima Mbeya City watafungwa mchezo huo hata kwa bao la NAPE. Kwa sisi tunaoujua unazi wake kwa Yanga hatukyshangazwa na uvunjwaji na upindishaji wake wa sharia za soka. Boban na Yondan walistahili kadi nyekundu lakn alushindwa kutoa, unajua ni kwanini? Nitafute nikwambie.

    ReplyDelete
  2. Mimi binafsi kwa kadiri nilivyomfuatilia refa wa mechhi ya Yanga na Mbeya City hata kabla ya mechi hiyo, nilijua tu lazima Mbeya City watafungwa mchezo huo hata kwa bao la NAPE. Kwa sisi tunaoujua unazi wake kwa Yanga hatukyshangazwa na uvunjwaji na upindishaji wake wa sharia za soka. Boban na Yondan walistahili kadi nyekundu lakn alushindwa kutoa, unajua ni kwanini? Nitafute nikwambie.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic