Pierre Aubameyang amebeba tuzo ya mwanasoka bora Afrika kwa mwaka 2015 na kumpiga kumbo Yaya Toure.
Toure alibeba tuzo hiyo mara tatu mfululizo na kama angechukua leo ilikuwa ni mara ya nne mfululizo ambayo ingekuwa ni rekodi.
Aubameyang anekipiga katika kikosi cha Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon ambayo yeye ni nahodha.
Tuzo hizo zimefanyika jijini Lagos nchini Nigeria na kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu katika soka barani Afrika.
Yaya anayekipiga anayekipiga katika kikosi cha Man City alishika nafasi ya huku ikienda kwa Andre Ayew ambaye aliongozana na baba yake, Abeid Pele.
0 COMMENTS:
Post a Comment