January 3, 2016

PROMOTA WA PAMBANO HILO, JAY MSANGI (WA PILI KUSHOTO) AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI JIJINI DAR, LEO. KUSHOTO NI KOCHA WA CHEKA, ABDALLAH SALEH 'KOMANDO', RAIS WA TPBO, ABDALLAH USTAADHI NA MENEJA WA CHEKA.

Pamoja na kushindwa na Thomas Mashali ‘Simba Asiyefugika’, bondia namba moja nchini, Francis Cheka, anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na bingwa wa Bara la Ulaya, Geard  Ajetovic raia wa Uingereza katika pambano la kugombania  mkanda wa ubingwa wa WBF  Intercontinental linalorajiwa kufanyika Februari 27, mwaka huu kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar.

Cheka ambaye hivi karibuni alipoteza dhidi ya Mashali katika pambano lisilokuwa la ubingwa lililofanyika mkoani Morogoro, atacheza pambano hilo huku akiwa na kumbukumbu ya kuwahi kuchapwa na bondia huyo mwenye asili ya Serbia katika pambano lililofanyika nchini Uingerezea miaka kadhaa iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Saalam, promota wa pambano hilo, Juma Msangi ‘Jay Msangi’ alisema kuwa pambano hilo la kugombania ubingwa ambalo ni maalum kwa ajili ya Cheka ili aweze kulipiza kisasi cha kupigwa na mkalia huyo wa Ulaya huku likitarajia kusimamiwa na Shirikisho la Ngumi za Duniani (WBF).


“Tumeamua kundaa pambano hili kwa ajili ya Cheka kurudiana na Ajetovic ambaye alimchapa nchini Uingereza miaka iliyopita, sasa tunaamini safari hii itakuwa ni zamu ya Cheka kulipiza kisasi kwa sababu atacheza katika ardhi ya nyumbani mbele ya Watanzania na litasimamiwa na Rais wa WBF.

Lakini kwa upande wa kocha wa bondia huyo Abdallah Saleh ‘Komando’ alisema kuwa: “ Cheka yupo sawa kabisa, ana nguvu za kutosha licha ya kwamba alipoteza pambano mwaka uliopita  dhidi ya Mashali lakini naomba waandaji wa pambano hili watufanyie mpango wa kuhakikisha tunapata kambi ya muda mfupi nje ya nchi  ambayo itasaidia kumuweka vizuri zaidi kabla ya pambano hilo”.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic