January 1, 2016


Kazi sasa, mambo yanazidi kuonekana magumu baada ya klabu ya TP Mazembe kusema ingependa kuona mshambuliaji Mbwana Samatta anajiunga na Standard Liege na Gent.

Uamuzi huo wa Mazembe, wazi unaonekana kumchanganya Samatta ambaye tayari alifanya mazungumzo na Gent na kumalizana nayo, alichokuwa anasubiri ni vigogo hao wa Ubelgiji kubalizana na TP Mazembe.

Lakini kwa hali ilivyo inaonekana TP Mazembe, umeshindwa kumalizana na Gent na sasa wameamua ajiunge na Liege ambayo wamezungumza na kuelewana.

Hali hiyo imezua mzozo mkubwa katika mkutano kati ya TP Mazembe na Samatta aliyekuwa na meneja wake, Jamal Kisongo. Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam, haukuisha kwa kila upande kukubali makubaliano ya upande mwingine.

Hali hiyo imezua mkanganyiko kwa kuwa Mazembe hawaelezi sababu za msingi za Samatta kuachana na Gent na kujiunga na klabu ya Liege.

Liege inashika nafasi ya 8 katika Ligi Kuu Ubelgiji huku Gent wakiwa wanaongoza ligi hiyo yenye timu 16.


Lakini Gent  tayari wamemalizana na Samatta na kumuweka dau mezani lakini Mazembe wanaonekana kutokukubaliana na hilo.

2 COMMENTS:

  1. Tatizo nini samata akaushe tuu. Asisaini mkataba huo wa liege asubiri mkata wake uishe awe mchezaji huru aende anapopataka wasimzingue

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic