January 24, 2016



Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, leo amesema aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha alikuwa akificha barua za kiungo Haruna Niyonzima alizokuwa akiziwasilisha kwa ajili ya utetezi au taarifa kuwa anatakiwa timu ya taifa ya Rwanda.

"Baada ya kuupitia uamuzi wa Kamati ya Nidhamu kuamua sababu kuvunja mkataba kati ya klabu Yanga na mchezaji Haruna Niyonzima, nilihisi kulikuwa kuna kasoro hasa kwa mchezaji anayelipwa mshahara wa Sh milioni 6 anaweza vipi kupuuzia maisha yake na kuanzisha mgogoro usiokuwa na tija kwa maisha ya kipato. 

"Niliamua uchunguzi wa ndani ufanyike katika suala hilo zima na mwisho, Jonas Tiboroha alibainika kuwa hakuwasilisha ushahidi ya mawasiliano sahihi kwa Kamati ya Nidhamu kuhusiana na Haruna Niyonzima, hali iliyosababisha kamati kuchukua uamuzi ambao haukuwa sahihi kwa sababu;

"Kulifanyika mambo ambayo hayakuwa sahihi, mfano barua za Niyonzima kutoka kwa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa) ambazo zilitumwa kwa TFF na kupokelewa kama ambavyo Azam FC walipokea ya mchezaji wao kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu wao. 

"Lakini barua ya Niyonzima kuja Yanga, ilionekana haikupokelewa kama ilivyokuwa kwa barua yake ya utetezi na ile ya kuomba radhi alizoandika, nazo zilipokelewa lakini hazikuwasilishwa kwenye kamati ya nidhanmu na hili, mhusika ni Tiboroha. Ukiachana na kamati kufanya uamuzi usio sahihi, hili pia limemjengea mchezaji chuki kubwa kwa wanachama na mashabiki. 




FERWAFA ILITOA OMBI LA NIYONZIMA KWENDA KUCHEZA MICHUANO YA KIMATAFA KUWANIA KUCHEZA KOMBE LA DUNIA DHIDI YA LIBYA

FERWAFA WALIMUOMBEA NIYONZIMA RUHUSA KWA AJILI YA CHALENJI, AWALI ILIELEZWA ALIKWENDA KUSHIRIKI CHALENJI BILA YA RUHUSA...


BARUA NYINGINE YA NIYONZIMA INAYOELEZWA KUFICHWA...

KITENGO CHA TIBA, TIMU YA TAIFA YA RWANDA KILIANDIKA KUHUSIANA NA MAJERAHA YA NIYONZIMA

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic