January 24, 2016



Kocha wa Simba, Jackson Mayanja amesema vijana wake wanamvutia kwa kuwa wanakamata mafunzo yake haraka.

Lakini akasema anataka kuongeza kasi zaidi ya Simba linapofikia suala la ushambuliaji katika mechi zao.

“Maelekezi wanafuata, lakini nafikiri jambo zuri ni kuona timu inakuwa na kasi zaidi kila tunapokwenda kushambulia.

“Shambulizi lazima liwe hivi; kwa kushitukiza au kama mtu analiona lazima liwe na kasi. Kushambulia polepole hakuwezi kuwa shambulizi sahihi,” alisema.


“Mpira kila siku unabadilisha mambo kutokana na mnachojifunza, tunaendelea kubadilisha mambo mazoezini na kuyafanyia kazi kwenye mechi,” aliongeza Mayanja ambaye ameiongoza Simba katika mechi tatu na kushinda zote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic