January 1, 2016


Baada ya Mwadui FC kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga,  Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema kinachoiponza Simba ni kucheza pasi nyingi zisizo na faida.

 Julio aliyewahi kucheza na kuifundisha Simba alisema: “Simba ni timu kubwa na wanashindwa kupata matokeo mazuri kutokana na kuwa wanapiga pasi nyingi mpaka wanaudhi ilhali hawafiki langoni kwa wapinzani wao, sasa hizo pasi za nini wakati hata golini hawafiki?” alihoji Julio na kuongeza:


Aidha, alisema kwa mwanendo uliopo sasa, Simba haiwezi kuwa katika mbio za kuwania ubingwa badala yake ijipange katika msimu ujao kutokana na timu hiyo kusuasua katika ligi.

Hata hivyo, Julio alikiri kwamba Ligi Kuu Bara ni ngumu kutokana timu kupishana pointi kwa kiasi kidogo sana kuanzia kileleni hadi chini.


SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Mpuuzi huyo simba ilipocheza na mwadui simba ilikolini kwa mwadui mara ngapi? goli ngapi zilikua offside. Huyo julio sio mzima na bado hajapata sababu zinasofanya simba ishingwe kushinda. Simba haina kiungo mshambuliaji mzuri anayeweza kutoa pasi za mwisho kwa wakati na sahihi. Na ndio maana utakuta simba inapata offside nyingi kwa kuwa mshambuliaji anapata nafasi ya kutoka butkiungo anachelewa kuupenyeza mpira kwa wakati

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic