January 19, 2016



Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana mwishoni mwa wiki na kupitia kesi, mashauri mbalimbali kuhusiana na usajili na mikataba ya wachezaji na viongozi mbalimbali chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili Mandi.

Kamati ilipata pingamizi kipindi cha pingamizi baada ya usajili kufungwa tarehe 15 Desemba 2015, wiki ya tarehe 16-22 Desemba.

Kwamba kamati imeona usajili ulifungwa tarehe 15 Desemba 2015, na kwamba tarehe 16 hadi 22 Desemba 2015 ni muda uliowekwa kwa ajili ya kuweka pingamizi. Katika muda huo klabu ya Kurugenzi ilileta pingamizi dhidi ya mchezaji George E. Mpole. 

Na kwamba kamati hii ilikaa tarehe 23/12/2015 pamoja na maamuzi mengine kamati iliamua kwamba klabu ya Kimondo FC isimchezeshe mchezaji husika yaani George Enock Mpole hadi watakapoelewana na Kurugenzi ya Mafinga na kwamba watakapokubaliana watatoa taarifa TFF ili TFF imruhusu mchezaji huyo aendele kucheza.

Na kwamba barua iliyowasilishwa na Kimondo mbele ya kamati hii kwamba walikubaliana tarehe 17/12/2015 haiwezi kuwa ushahidi mzuri kwa kuwa malalamiko yalikuwepo na kamati ilikaa tarehe 23/12/2015 na endapo kungekuwa na makubaliano katika hali ya kawaida kungekuwa na taarifa ambayo haikuwepo.

 Na kwamba hata baada ya taarifa rasmi kutolewa na TFF ya kwamba mchezaji amewekewa pingamizi na hatakiwi kucheza  hivyo wasimtumie mpaka wakikubaliana na klabu yake yaani Kurugenzi FC, hawakuwahi kutoa taarifa yoyote hivyo basi klabu ya Kimondo S.C imemchezesha mchezaji ambaye amesimamishwa na TFF.

Kanuni ya 42 (9) inasema kama ifuatavyo;

“Timu yoyote ambayo itamchezesha mchezaji aliyechini ya adhabu ya kufungiwa /kusimamishwa au ambaye ametakiwa kulipa faini kwa maelekezo maalumu na hajalipakwa mujibu wa kanuni hii itapoteza mchezo huo na timu pinzani itapewa ushindi” Kwa mujibu wa kanuni hii kamati inatoa adhabu dhidi ya timu ya Kimondo SC katika mchezo uliochezwa tarehe 26/012/2015 dhidi ya Lipuli FC.

Na kwamba timu ya Lipuli ndiyo itakuwa mshindi wa mchezo huu, hivyo itapewa pointi tatu (3) na magoli matatu (3).

Mchezaji huyo ataendelea kusimamishwa mpaka TFF itakapojiridhisha ya kwamba taratibu za usajili zimekamilika. Kurugenzi ndio itakayotoa taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya kamati.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic