January 11, 2016


Baada ya Mchezaji Bora wa Afrika, Mbwana Samatta kuondoka TP Mazembe na kusaini Genk ya Ubelgiji, ‘pacha’ wake, Thomas Ulimwengu ameweka wazi kuwa naye yupo njia kuondoka Mazembe na jicho la kwanza limetua katika Klabu ya Saint Etienne ya Ufaransa.

Ingawa Samatta safari yake haijaiva kisawasawa kutokana na Mazembe kumuwekea kauzibe, bado ana asilimia 98 za kukipiga na mabingwa hao mara tatu wa Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Kumekuwepo na tetesi za Ulimwengu kutakiwa na Besiktas ya Uturuki, hata hivyo yeye ameibuka na kusema dili jingine lipo Ufaransa ambako amesema bado mchakato unaendelea.

“Nampongeza Samatta kwa hatua aliyofikia, anaondoka na mimi niko njiani, nitaondoka Mazembe…kuna timu zinanihitaji kama Saint Etienne lakini bado ni suala la kimchakato kidogo,” alisema Ulimwengu.


Awali, meneja wake, Jamal Kisongo  aliliambia gazeti hili kuwa kuna timu zipo nyingi zinazomhitaji Ulimwengu lakini kikwazo kikubwa ilikuwa ni safari ya Samatta kuondoka Mazembe ambayo ilikuwa na mchakato mzito sana kwani Wakongo hao hawakuwa tayari kumuachia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic