Kocha aliyetupiwa virago Simba, Dylan Kerr ameibukia katika klabu ya Manchester City.
Kerr ametupia picha mtandaoni akiwa katika ofisi za klabu ya Manchester City pamoja na uwanja wa klabu hiyo wa Etihad.
Hata hivyo haikujulikana mara moja, alikuwa amefika kwenye ofisi za klabu hiyo huku akionekana na baadhi ya maofisa wa Man City kwa sababu zipi.
Juhudi za kumsaka Kerr hazijafanikiwa, lakini tunaendelea kumsaka ili kujua alikuwa katika matembezi ya kawaida tu au kuna jambo.
Huko ni nyumbani kwao na hao maofisa wa etihad ni wenzake,kwani wewe huwezi kwenda jangwani au Msimbazina kuzungumza na maafisa wa Yanga au Simba?Sidhani kama kuonekana kwake hapo Etihad ni habari.Labda Ungemuona Guadiola etihad hiyo ingeweza kuwa habari kwa sababu ndiye kocha anayesubiriwa kuanza Kazi hapo Etihad
ReplyDelete