Mwamuzi Jonesia Rukyaa sasa ndiyo gumzo katika mitandao yote inayozungumzia soka nchini.
Wadau wanajadili kuhusiana na uwezo wake na wanavyoamini itakavyokuwa mara tu baada ya kutangazwa kuwa atachezesha mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Simba.
Rukyaa aliwahi kuchezesha mechi ya Nani Mtani Jembe, Simba ikashinda kwa mabao 2-0, ingawa awali alishindwa kuudhibiti mchezo.
Mwishoni, alifanikiwa kutulia na mambo yakaenda vizuri hadi mwisho. Lakini wengi wamekuwa na hofu kama ataliweza pambano hilo.
Mwamuzi huyo kutokea mkoani Kagera ametangazwa leo na TFF kuwa atachezesha mechi hiyo.
Amepewa tena waamuzi wasaidi kutoka Tanga kwa ajili ya pambano la watani linalosubiriwa kwa hamu kubwa kuupita kifani.
Waamuzi hao wasaidizi kutoka Tanga ni Josephat Bulali na Samwel Mtenzu.
0 COMMENTS:
Post a Comment