Wachezaji sita wa Simba, walicheza wakiwa na kadi mbili za njano katika mechi dhidi ya Stand.
Katika mechi hiyo ambayo Simba ilishinda kwa mabao 2-1, nyota Hamisi Kiiza na Ibrahim Ajib nao walikuwa na kadi mbili za njano na kama wangekosea tu, basi, wangeikosa mechi dhidi ya Yanga.
Wachezaji wengine ni Juuko Murishid, Mwinyi Kazimoto, Hassan Kessy na Abdi Banda.
Hata hivyo wachezaji wote hao walifanikiwa kuepuka adhabu hiyo kwa kutopewa kadi huku Kiiza akifunga mabao yote mawili na kuangusha Stand kwao Kambarage.
Meneja wa Simba, Abbas Ally, ili kujua ukweli wake ambapo alisema kuwa timu hiyo haina mchezaji yeyote mwenye kadi tatu za njano isipokuwa ina wachezaji sita wenye kadi mbili za njano.
“Hatuna mchezaji yeyote mwenye kadi tatu za njano ila tuna wachezaji kama sita waliokuwa na kadi mbili za njano ambazo walizipata kabla ya mechi yetu na Stand United,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment