February 17, 2016

CANNAVARO

Bosi wa benchi la ufundi la Yanga, Hans van Der Pluijm, amegoma kuzungumzia nafasi ya beki na nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ndani ya kikosi chake cha kwanza baada ya beki huyo kurejea akitokea katika kipindi cha majeruhi.

Pluijm raia wa Uholanzi alikuwa anamtumia Cannavaro katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo sambamba na Kelvin Yondani kabla ya kuumia ambapo nafasi yake ikachukuliwa na Mtogo, Vincent Bossou.

 Pluijm alisema kuwa kwa sasa ni mapema kuanza kuzungumzia nafasi ya beki huyo baada ya kurejea akitokea majeruhi ambapo anampa muda wa kujiweka sawa kabla ya kumrejesha ndani ya kikosi hicho.

PLUIJM NA MWAMBUSI
“Kwa sasa ni mapema kuanza kuzungumzia nafasi ya Cannavaro kwenye ‘first xi’ kwani kama unavyojua ndiyo kwanza amerejea kutoka nje alipokuwa akisumbuliwa na majeraha ya kisigino.


“Nitakachokifanya kwa sasa ni kumpa muda wa kujinoa zaidi na kujiweka sawa kwa ajili ya kurejesha makali yake kwani kama unavyojua hajacheza kwa kipindi kirefu, hivyo atafanya mazoezi hayo ya kujiweka sawa kabla ya baadaye kumrejesha,” alisema Pluijm.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic