Kocha Mkuu wa Prisons, Salum Mayanga amesema pamoja na kutocheza mechi moja ya ligi, bado wana uhakika wa kufanya vizuri leo, dhidi ya Yanga.
Prisons ni wenyeji wa Yanga kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Mayanga amesema wamejiandaa vizuri licha ya kwamba walikosa mechi moja dhidi ya Azam FC ambayo iliomba kwa TFF kwenda kushiriki michuano ya muda nchini Zambia.
“Kweli kukaa kucheza kunaweza kupoteza ile hali ya mwendo wa timu, lakini tumekosa mechi moja tu. Naamini haiwezi kutuzuia kwenda kwa mwendo wetu.
“Tumejiandaa vya kutosha na tunataka kufanya vizuri kwenye mechi ya leo na pia kuendelea kufanya vizuri. Ninashukuru vijana wako vizuri na tayari kwa mechi ya leo,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment