February 3, 2016


Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amekiri kuwa majeruhi ni tatizo kubwa kwao, lakini akasisitiza wana kila sababu ya kupambana na kufanya vizuri katika mechi yao ya leo dhidi ya Prisons.

Prisons inayofundishwa na Kocha Salum Mayanga ni wenyeji wa Yanga kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao Yanga itawakosa ni pamoja na nahodha Nadir Ali Haroub, Haji Mwinyi, Thabani Kamusoko walio majeruhi pia Kelvin Yondani mwenye kadi nyekundu.

"Suala la majeruhi mfululizo limetupa wakati mgumu sana, tunajua haya ni mambo yanayoweza kutokea wakati wowote katika soka. Lakini kitu cha mwisho ni mwaka lazima tupambane na kushinda.

"Walio majeruhi na walikuwa wanacheza katika kikosi cha kwanza ni wachezaji muhimu na tunawahitaji, lakini walio fiti ni muhimu sana na tunawategemea.

"Kikubwa ni kuomba tuwe salama hadi wakati wa mechi ili tuweze kupambana kwa ajili ya klabu na tunacholenga ni kupata ushindi," alisema Mwambusi, kocha wa zamani wa Mbeya City.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic