February 24, 2016



DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 85 hadi 90 zaidi mpira unachezwa katikati mwa uwanja huku kukiwa na mashambulizi duni kabisa na Yanga kwa aina fulani wanaonekana kuridhika na mabao hayo mawili

Dk 84, Mwashiuya anapiga chenga safi ndani ya boksi la JKT lakini anashindwa kumalizia

Dk 79, Mnubi anachonga kona nyingine safi kabisa, Cannavaro anapiga kichwa na kuokoa
Dk 78, JKT wanafanya shambulizi jingine na kupata kona baada ya Kamusoko kuokoa mpira. Hii ni kona ya sita kwao. Mnubi anachonga kona, kona tena

Dk 77, JKT Mlale wanafanya shambulizi, Yanga wanaokoa na kuwa kona. Inachongwa, Yanga wanaokoa na kuwa kona tena, lakini Omary anachonga kona ya hovyo kabisa na unatoka nje. Goal Kick

Dk 75, Yanga wanafanya shambulizi kali lakini Ngoma akiwa katika eneo la hatari anaanguka mwenyewe

Dk 70, Mwashiuya anapiga shuti kali lakini kipa JKt anafanya kazi ya ziada, anaokoa na kuwa kona inayochongwa na Thabani KamusokoKADI Dk 65, Oscar Mhagama anamwangusha Busungu na kulambwa kadi ya njano
Dk 59 na 62, Yanga wanaonekana kutulia zaidi katika kiungo na kutawala zaidi hasa baada ya mabadiliko ya Kamusoko

SUB Dk 59, Yanga inamuingiza Malimi Busungu kuchukua nafasi ya Bonga

GOOOOOOO Dk 58 Kamusoko anafunga bao kwa ulaini katikati ya mabeki wa JKT baada ya kuunganisha pasi nzuri ya MWashiuya
SUB Dk 55, Yanga wanamtoa Telela aliyeumia na nafasi yake inachukuliwa na Thabani Kamusoko

Dk 52 mchezaji mmoja anamgonga Telela kwa nyuma upande wa Medula Blangata, anatibiwa uwanjani lakini anatolewa nje kwa ajili ya matibabu zaidi

Dk 51, Ngoma anaanguka na mwamuzi anasema ni faulo ingawa inaonekana aliteleza mwenyewe
DK 47, Yanga waanza kwa kushambulia, lakini hata hivyo shuti la MSuva halilengi lango
SUB Dk 46 Yanga inamtoa Matheo Simon na nafasi yake inachukuliwa na Donald Ngoma

MAPUMZIKO
Dk 45+2 Songa wa JKT anaingia vizuri na mpira, anapiga krosi safi lakini Dida anawahi na kudaka
DAKIKA +4
Dk 45, kipa Murish analala tena, hata hivyo hakuwa amegongana na Nonga kama anavyotaka kuonyesha. Huenda anaendelea kupoza presha ya Yanga

Dk 43, kipa Murish anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira kichwani mwa NongaDk 41, JKT Mlale wanaonekana kupunguza presha ya Yanga waliochangamka kwa kucheza taratibu
Dk 39, Yanga wanaonekana kuchangamka, Twite anapiga shuti kali kabisa, lakini ni goal kick
GOOOOOO Dk 38, Mwashiuya anaingia kwa kasi na kupiga krosi nzuri kabisa na Nonga anaunganisha kwenye lango lililo wazi likimtazama

Dk 37, Alex Seti anapokea mpira wa kona akitokea pembeni mwa uwanja, anapiga shuti kali kabisa linatoka nje kidogo
Dk 34, kipa Noel Murish yuko chini pale, watu wa huduma ya kwanza wanaingia kwa ajili ya kutoa matibabu
Dk 33, Mwashiuya anaingia vizuri na kupiga krosi nzuri, Msuva anaunganisha lakini mpira unagonga mwamba na kuokolewa

Dk 28, Nonga anaingia vizuri kabisa baada ya kupokea pasi nzuri ya MSuva lakini shuti lake linapita juuu
GOOOOOOO Dk 21 Mgandila Shabani anaandika bao safi kabisa baada ya kupewa pasi kutoka pembeni mwa uwanja

Dk 13, JKT Mlale wanafanya shambulizi jingine, lakini washambulizi wake wanaonekana kuwa na hofu

Dk 10, JKT Mlale nao wanapata kona baada ya kushambulia, lakini wanapiga kona ambayo haina macho
Dk 9, Msuva anapiga krosi nyingi kali lakini mpira unaokolewa na kuwa kona

Dk 7, Nonga anapiga mpira unaokwenda langoni unaokolewa na kuwa kona isiyo na mashara
Dk 6 Msuva anaingia vizuri katika eneo la hatari lakini krosi anayopiga inakuwa haina macho
Dk 4, Seti anawazidi mbio mabeki Yanga lakini shuti lake linababatiza na kuwa kona isiyo na faida

Dk 2, Yanga wanakuwa wa kwanza kuingia katika lango la JKT, krosi ya MWashiuya lakini kipa anawadi anadaka

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic