February 24, 2016

Ageard Ajetovic

Bondia wa  kimataifa, Ageard Ajetovic raia wa Serbia amesema kuwa amekuja nchini kufanya kazi mmoja tu ya hukakikisha anamchapa mapema kabisa mpinzani wake  Franacis Cheka ‘SMG’  tena ikiwezekana kwenye raundi ya tano.

Cheka na Ajetovic wanatarajia kupanda ulingoni Jumamosi ya wiki hii kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, katika pambabo la kugombania Ubingwa wa Dunia WBF Intercontinetal.


Akuzungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Ajetovia ambaye amekuja na kocha wake Aksu Sahhaydar alisema kuwa nafahamu kuwa Cheka ni bondia mzuri lakini atahakikisha anaitumia nafasi hiyo kufumndisha mchezo huo kwa kuwa tayari ameshakuwa mzee ‘babu’.

“Nimewahi kuja kwa sababu ya kutaka kuzoeza mazingira kabla ya  siku ya Jumamosi kupanda ulingoni dhidi ya Franci Cheka kwa sababu natambua kama ni bondia mzuri lakini  nimekuja kwa kazi ya kuhakikisha namfundisha namna ya kucheza ngumi kutokana na umri wake kuwa ni mkubwa.



“Mapema tu,  nitakuwa nishamaliza pambano, nadhani katika raundi ya  nne au tano  kazi yangu iwe imeshamalizika kwa sababu Chaka siyo mgeni kwangu na nilishampiga nchini  Uingereza mwaka 2008  hivyo hakuna kitakachonishinda ila siwezi kusema kama itakuwa ni KO,” alisema Ajetovic.


 Lakini kwa upande wa  upande wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Advance Security, Juma Ndambile ambaye pia ni meneja wa Cheka alisema kuwa wameamua kuwashirikisha mabondia chipukizi ambao watacheza  mapambano ya utangulizi siku hiyo ni  Mohammed Bakari vs Cosmas Cheka, raundi nane.

Mustapha Dotto atazipiga na Mohammed Matumla, pia kwa raundi nanewakati Mada Maugo atacheza na Baraka Mwakansope badala ya Dulla Mbabe huku LuLu Kayage akitarajia kucheza na  Mwanne Haji pambano la  raundi Sita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic