Zile taarifa kwamba mwamuzi, Jonesia Rukyaa alitekwa baada ya kuelezwa simu yake haikuwa ikipatikana, zimeelezwa kuwa si za kweli.
Jonesia ni mwamuzi kutoka mkoani Kagera ambaye amepewa jukumu la kuchezesha mechi ya watani, Yanga na Simba, Jumamosi.
Tayari taarifa za yeye kupewa kuchezesha mechi hiyo imekuwa ni gumzo kubwa sehemu mbalimbali nchini.
Taarifa zinaeleza, Jonesia alikuwa njia kutoka Bukoba kwenda jijini Dar es Salaam, hivyo ilikuwa si rahisi simu yake kupatikana kutokana na tatizo la mawasiliano.
Lakini redio moja, leo mchana ilieleza kwamba mwamuzi huyo hakuwa akipatikana, hivyo kukawa na hofu huenda alitekwa.
Hata hivyo, watangazaji wake hawakuwa na data za kutosha kuhusiana na tukio hilo zaidi ya kusema simu yake haikuwa ikipatikana kabisa na ndugu zake walisema hawakujua alipokuwa akipatikana.
Lakini rafiki wa karibu wa Jonesia amezungumza na SALEHJEMBE na kusema Jonesia alikuwa njiani kutoka Bukoba.
“Ninachojua aliondoka Bukoba leo kuja Dar es Salaam, hivyo suala la kutekwa si kweli,” alisema rafiki huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment