Robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho ya Azam Sports HD itapangwa kwa mtindo wa droo ambao utakuwa hadharani.
Taarifa za ndani kutoka TFF umeeleza ndani ya leo, kesho au keshokutwa, suala hilo litafanyika hadharani na hii inaweza kusababisha watani wa jadi Yanga na Simba kukutana tena.
Wakati wa upangaji wa ratiba, hauwezi kujua nani anakutana na nani. Uamuzi huo unaonekana kufuata zaidi mfumo wa michuano mingine mikubwa kama vile Kombe la FA la England.
Kama Yanga na Simba hazitakutana, pia bado kuna "hatari" ya Azam FC kukutana na Yanga au Simba, jambo ambalo kwa wanaopenda michuano hiyo kuwa na utamu zaidi, wangependa zikutane mwishoni, angalau kuanzia nusu fainali.
0 COMMENTS:
Post a Comment