March 11, 2016


Baada ya kukaa nje kwa takriban mwezi mmoja akiuguza majeraha ya nyama za paja, straika wa Simba, Mkenya, Paul Kiongera, amesema tayari amepona na amerejea akiwa na kasi yake kama zamani.

Kiongera alisajiliwa na Simba msimu uliopita kabla ya kupelekwa kwa mkopo katika Klabu ya KCB ya Kenya, katikati ya msimu huu alirudishwa ndani ya kikosi cha Simba lakini bado hajaonyesha makali yake kama alivyokuwa KCB kutokana na kusumbuliwa na mejeraha ya mara kwa mara.

Jumatatu na Jumanne ya wiki hii, Kiongera alifanya mazoezi na kikosi cha Simba kwenye Ufukwe wa Coco kabla ya kuhamia katika Uwanja wa Boko jijini Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa jana Alhamisi wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda.
  
Meneja wa timu hiyo, Abass Ally, amesema kwa sasa Kiongera yupo fiti na kama kocha ataridhishwa na kiwango chake mazoezini, anaweza kumtumia kwenye michezo ijayo.


Kiongera amesema: “Nipo vizuri kwa sasa, nimejipanga kwa lolote lile ikiwemo kugombania namba kikosini, kwani naamini hakuna sehemu isiyokuwa na ushindani, kutokana na kukaa nje kwa muda mrefu, nimepanga kufanya mazoezi kwa nguvu ili kumshawishi mwalimu aweze kunipa namba.” 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic