March 28, 2016


Anga ya michezo hasa ule wa soka kwa Afrika Mashariki umepata msiba mkubwa baada ya kipa Abel Dhaira, kufariki dunia nchini Iceland alikokuwa anasumbuliwa na kansa ya utumbo.

Dhaira amefariki jana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema amepokea kwa mshituko mkubwa kifo cha kipa huyo wa zamani wa Simba ya Tanzania, URA, Express na timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.

Aidha, Museveni amesema serikali yake itagharimia kila kitu ikiwemo kuusafirisha mwili wake pamoja na mazishi, huku akiwapa pole wanafamilia wa Dhaira na familia yote ya wapenda michezo katika kipindi hiki cha majonzi.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV