April 27, 2016


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekiri mwamuzi Abdallah Kambuzi amechezesha chini ya kiwango mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA kati ya Yanga na Coastal Union wikiendi iliyopita.

Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ulivunjika kabla ya muda wa nyongeza kumalizika baada ya mashabiki wanaodaiwa kuwa ni wa Coastal kurusha mawe uwanjani.

Hadi mchezo huo unavunjika dakika ya 105, Yanga ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-1. Mashabiki hao waliorusha mawe walikuwa wakipinga bao la pili la Yanga lililofungwa na Amissi Tambwe kwa madai alikuwa ameunawa mpira wakati akifunga.

Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Chama, alisema Kambuzi ni mmoja wa waamuzi wazuri nchini lakini alikosea baadhi ya vitu katika mchezo huo. 

“Hatukatai kama inawezekana Kambuzi alivurunda kwenye ule mchezo kwani tunajua kabisa kuwa waamuzi wetu nao huwa wanafanya makosa kwenye baadhi ya mechi lakini hiyo haimaanishi kuwa ni wabaya.

“Wakati mwingine mtu anakosea katika hali ya kibinadamu na ikibainika huwa tunampa adhabu, waamuzi wetu ni kama unavyowaona wachezaji vile kuna siku mpira huwa unamkataa.


“Kambuzi atachunguzwa kwa mambo aliyofanya japo tunatambua kuwa ni mmoja kati ya waamuzi wazuri wa daraja la kwanza la uamuzi,” alisema Chama. Kambuzi hivi karibuni ataingia kwenye orodha ya waamuzi wanaotambulika na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

1 COMMENTS:

  1. Saleh usitake kumponza huyo mwanachama mwenzio wa Simba(Salum Chama),kamwe hawezi kusema eti mwamuzi alichemsha kwa mujibu wa ibara ya 15 ya maadili ya waamuzi.Kwani kufanya hivyo ni kumtenganisha na chama chake na kumfanya kufungiwa miezi isiyopungua sita.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic