April 27, 2016Beki wa kati wa Simba anayekipiga kwa mkopo Mwadui FC, Joram Mgeveke, amesema heshima anayopewa na kocha wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, inamfanya ayafurahie maisha ya timu hiyo na kutotamani tena kurudi Simba.

Mgeveke ambaye alijiunga na Simba misimu miwili iliyopita akitokea Lipuli ya Iringa, mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo anaona kwa hali ilivyo, ni bora abaki Mwadui.

Mgeveke alisema Julio ndiye anamfanya asiifikirie Simba kwa kuwa mara kwa mara amekuwa akimpa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

...WAKATI AKIWA SIMBA

“Huku nilipo ‘nainjoi’ sana kama kucheza nacheza tena kikosi cha kwanza, mimi naona ni bora nibaki hukuhuku, naipenda Simba lakini huku napapenda kwani Kocha Julio ananiamini na pia hakuna presha.

“Mkataba wangu na Simba unaisha mwishoni mwa msimu huu, hivyo nipo huru kufanya mazungumzo ya mkataba mpya lakini mimi naona ni bora nibaki Mwadui na siyo kurudi Simba,” alisema Mgeveke.

Mgeveke ni miongoni mwa wachezaji walioibuliwa na mpango wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wa kutafuta wachezaji mbadala wa Taifa Stras na kuitwa Taifa Stars Maboresho. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV