April 27, 2016


Beki wa kati wa Yanga, Vincent Bossou, amesema mashabiki wa Coastal Union ya Tanga walitaka kuwaua uwanjani kutokana na vurugu walizokuwa wakifanya Jumapili iliyopita.

Vurugu hizo za mashabiki hao waliodhaniwa kuwa wa Coastal, zilisababisha mwamuzi msaidizi wa mechi hiyo ya nusu fainali ya Kombe la FA kati ya Yanga na Coastal, Charles Simon kujeruhiwa na jiwe kichwani. 

Yanga walikutana na Coastal Union katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ambao ulivunjika dakika ya 115 baada ya Yanga kupata bao la pili.

Bossou ameliambia Championi Jumatano kuwa, wao kama wachezaji walikuwa kwenye wakati mgumu kufuatia mashabiki wa timu hiyo kuwarushia mawe ambayo kama yangewapata, usalama wao ungekuwa shakani zaidi.

 “Halikuwa tukio zuri hata kidogo kutokana na mashabiki wa Coastal Union kuanzisha fujo na kutupa mawe uwanjani ambayo yalikuwa yanatulenga sisi na baadhi yaliweza kumfikia Dida (Deogratius Munishi) na Oscar Joshua ambapo ile ilikuwa hatari sana kwetu.

“Mawe yale kama yangeweza kutupiga, hasa basi, madhara yangekuwa makubwa zaidi ya yale yaliyotokea na utaona kuwa tulitoka kwa kutumia basi letu ambalo liliingia uwanjani,” alisema Bossou, raia wa Togo.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic