April 27, 2016


Kocha Msaidizi wa Azam FC, Denis Kitambi, amepanga kukatisha mbio za Kocha wa Simba, Jakson Mayanja za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kitambi amesema njia pekee ya kuizuia Simba isitwae ubingwa ni kuhakikisha wanaifunga wikiendi hii kwenye mchezo wao wa ligi kuu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba ina pointi 57 katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi huku Yanga ikiongoza kwa kuwa na pointi 59 na Azam yenyewe ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 55.

Kitambi alisema kasi waliyonayo hivi sasa hawawezi kuipunguza na wanachoangalia ni kuhakikisha wanashinda mchezo huo ili kuipoteza Simba. 

“Tuna majeruhi wengi katika timu lakini wachezaji waliobaki wamejiandaa vya kutosha kuelekea mechi yetu dhidi ya Simba, yaani wapo vizuri.


“Kwa jinsi ligi ilipofikia hivi sasa kila mechi tunayocheza ni fainali kwetu kuona tunafanikiwa kupata pointi tatu katika kila mchezo,” alisema Kitambi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV